banner

The New Stuff

17 Views

CHAMA CHA CUF CHAMPONGEZA SHEIKH PONDA ISSA


Chama Cha Wananchi (CUF) kimetoa pongezi kwa Sheikh Ponda baada ya jana kuwataka Watanzania bila kujali itikadi zao na imani zao za dini kwa pamoja kushikamana kutetea na kulindwa kwa haki za binadamu, uhuru wa Kidemokrasia na utawala wa sheria.

Sheikh Ponda aMEsema hayo jana baada ya kumtembelea Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu jijini Nairobi anakopatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi mnamo Septemba 7, 2017 mjini Dodoma.

Kufuatia kauli hiyo wa Sheikh Ponda Chama Cha Wananchi CUF kimempa pongezi kiongozi huyo kwa uthubutu wake wa kusema ukweli na kukemea maovu mbalimbali ambayo yanaendelea nchini.

“Tunampongeza kwa kujitokeza katika kipindi hiki ambacho Watanzania na Viongozi wengi wa dini na kisiasa wamejazwa woga, wale waliokuwa mstari wa mbele kukemea maovu katika awamu zilizopita hivi sasa wamejitia upofu, ububu na uziwi. Tunampongeza kuelezea Umuhimu na Ulazima kwa Watanzania kuungana pamoja kutetea uwepo wa mfumo wa Haki, Demokrasia na Utawala wa Sheria kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” amesema Mbarala Maharagande.

Aidha Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF, Mbarala Mharagande amedai kuwa wao CUF wanatarajia viogozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, wasomi mbalimbali, waandishi wa Habari na wananchi kwa ujumla hawapaswi kukaa kimya bali wanapaswa kukemea mambo mabaya ambayo yanaendelea nchini, huku wakivitaka vyombo vya dola kutekeleza wajibu wao.

Recently Published

»

BARAKAH AKANUSHA KUMWAGANA NA NAJ

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amekanusha kumwagana ...

»

HATUTAMBUI URAIS WA KENYATTA – RAILA ODINGA

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Nasa, Raila Odinga ...

»

TUNDU LISSU AMPONGEZA NYALANDU KWA UJASIRI

Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu Lissu amempongeza ...

»

MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBER 1, 2017

...

»

EAC PLACES HARD STANCE OVER DONOR FUNDS MANAGEMENT

EAC Secretary General Ambassador Liberat Mfumukeko  told the first ...

»

SCORPION AKUTWA NA KESI YA KUJIBU

Mshtakiwa Salum Njwete, maarufu kwa jina la ‘Scorpion’ amekutwa ...

»

ETHIOPIA’S B787-9 MAIDEN TRIP TO ‘KIA’ A BOOST TO TOURISM IN TANZANIA

The Boeing touching down to Kilimanjaro International Airport (KIA) ...

»

ZITTO KABWE AACHIWA KWA DHAMANA KESI YA MAKOSA YA MTANDAO

Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ...

»

6,400 IMPORTED CHICKS TO FACE CULL – TANZANIAN GOVERNMENT

Authorities will destroy 6,400 chicks which were smuggled from Kenya ...

Shares
0

Your Cart