banner

The New Stuff

10 Views

RAIS MAGUFULI ATAKA WANAOPIKA DATA ZA SERIKALI WASHUGHULIKIWE


Rais John Pombe Magufuli amefunguka na kuvitaka vyombo vya dola nchini viwashungulikiwe watu ambao wamekuwa wakipika data za uongo za serikali na kuzichapisha sehemu mbalimbali na kusema watu hao wanapaswa kufikishwa mahakamani.
Rais Magufuli amesema hayo leo katika hafla ya kuwatunuku vyeti vya pongezi maaalum kwa wajumbe waliohusika kuchunguza kiwango, aina ya madini katika mchanga wa madini ambao ni makinikia. Rais Magufuli amesema kuwa kuna haja Waziri wa Sheria na vyombo vya dola kuangalia namna inavyowezekana kuwashughulikia watu ambao wanapika data.
“Niwaombe Watanzania wengi tofauti na wale wachache wanaopiga kelele muwapuuze, mtu ambaye anabadili data za serikali na kusema kuwa uchumi umeshuka nadhani wanapaswa kuchukuliwa hatua vyombo vya dola na wewe Profesa Kabudi ni Waziri wa Sheria muanze kuangalia watu wa namna hii ambao kwao kubadili Takwimu wanaona kitu kidogo.
“Nafikiri kuna sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 na kunakifungu kinasema mtu anayebadilisha Takwimu za serikali anaweza kufungwa hata miaka 2 jela, kwanini hatuvitumii hivi? Unakuta mtu anazungumza makusanyo ya serikali yameshuka wakati anajua kabisa si kweli” alisema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa mapato ya nchi hayajashuka ndiyo maana Serikali imeweza kununua ndege zaidi ya sita kwa mpigo, serikali imeweza kujenga barabara kwa fedha za ndani, na kusema serikali imeweza kujenga reli kwa kuwa uchumi wake ni mzuri.

Recently Published

»

BARAKAH AKANUSHA KUMWAGANA NA NAJ

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amekanusha kumwagana ...

»

HATUTAMBUI URAIS WA KENYATTA – RAILA ODINGA

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Nasa, Raila Odinga ...

»

TUNDU LISSU AMPONGEZA NYALANDU KWA UJASIRI

Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu Lissu amempongeza ...

»

MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBER 1, 2017

...

»

EAC PLACES HARD STANCE OVER DONOR FUNDS MANAGEMENT

EAC Secretary General Ambassador Liberat Mfumukeko  told the first ...

»

SCORPION AKUTWA NA KESI YA KUJIBU

Mshtakiwa Salum Njwete, maarufu kwa jina la ‘Scorpion’ amekutwa ...

»

ETHIOPIA’S B787-9 MAIDEN TRIP TO ‘KIA’ A BOOST TO TOURISM IN TANZANIA

The Boeing touching down to Kilimanjaro International Airport (KIA) ...

»

ZITTO KABWE AACHIWA KWA DHAMANA KESI YA MAKOSA YA MTANDAO

Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ...

»

6,400 IMPORTED CHICKS TO FACE CULL – TANZANIAN GOVERNMENT

Authorities will destroy 6,400 chicks which were smuggled from Kenya ...

Shares
0

Your Cart