banner

The New Stuff

13 Views

UWEZEKANO NI MDOGO WA KUFIKIA SULUHISHO MGOGORO WA QATAR – TILLERSON


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson amesema hakuna dalili ya upande unaoongozwa na Saudi Arabia kuanza majadiliano ya moja kwa moja na Qatar ili kuimarisha mahusiano.

Mwezi Juni Saudi Arabia na nchi kadhaa za Kiarabu zilisitisha mahusiano ya kidiplomasia na Qatar na kufunga mipaka ya ardhini, majini na angani kwa nchi hiyo, wakiituhumu kusaidia ugaidi na kuharibu hali ya utulivu katika eneo hilo.

Tillerson alizungumza hayo katika mkutano na waandishi wa habari jana Jumapili baada ya mkutano wa ana kwa ana na viongozi wa Saudi Arabia na Qatar.

Tillerson alisema alimshauri moja kwa moja Mwana mfalme wa Saudia Mohammed Bin Salman kuzungumza na Qatar lakini bado hakuna ishara ya dhati ya kwamba pande hizo zipo tayari kufanya majadiliano.

Marekani imekuwa mpatanishi kati ya pande hizo mbili ikijaribu kuunganisha mataifa hayo ya ghuba kwa mapambano dhidi ya kundi la wanamgambo wanaojiita Islamic State.

Recently Published

»

BARAKAH AKANUSHA KUMWAGANA NA NAJ

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amekanusha kumwagana ...

»

HATUTAMBUI URAIS WA KENYATTA – RAILA ODINGA

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Nasa, Raila Odinga ...

»

TUNDU LISSU AMPONGEZA NYALANDU KWA UJASIRI

Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu Lissu amempongeza ...

»

MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBER 1, 2017

...

»

EAC PLACES HARD STANCE OVER DONOR FUNDS MANAGEMENT

EAC Secretary General Ambassador Liberat Mfumukeko  told the first ...

»

SCORPION AKUTWA NA KESI YA KUJIBU

Mshtakiwa Salum Njwete, maarufu kwa jina la ‘Scorpion’ amekutwa ...

»

ETHIOPIA’S B787-9 MAIDEN TRIP TO ‘KIA’ A BOOST TO TOURISM IN TANZANIA

The Boeing touching down to Kilimanjaro International Airport (KIA) ...

»

ZITTO KABWE AACHIWA KWA DHAMANA KESI YA MAKOSA YA MTANDAO

Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ...

»

6,400 IMPORTED CHICKS TO FACE CULL – TANZANIAN GOVERNMENT

Authorities will destroy 6,400 chicks which were smuggled from Kenya ...

Shares
0

Your Cart